Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kununua Nyumba
OFISI INAYOHUSIKA
Shirika la Nyumba la Taifa

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Mchakato wa ununuzi wa nyumba umekusudiwa kuwa rahisi na usio na utata kadiri iwezekanavyo. Mchakato wa kuuza utaanza pamoja na uzinduzi wa mradi. Mara tu baada ya kutangaza kuwa mradi fulani uko tayari kuuzwa.

Utaratibu:

 • Chukua/pakua Fomu ya Maombi ya Kununua Nyumba
 • Uwasilishaji wa fomu ya maombi ya kununua nyumba
 • Lipa ada ya maombi na angalau 10% ya malipo ya awali (ya bei ya nyumba iliyoombwa)
 • Tathmini ya fomu za maombi ya kununua nyumba zilizochukuliwa
 • Kuorodhesha wote wanaotimiza vigezo vya ununuzi vilivyowekwa.
 • Kupeleka “barua ya ahadi ya kununua nyumba iliyoombwa” kwa waombaji wa kwanza waliotimiza masharti ya maombi (100%) ya kununua nyumba
 • Kupeleka “barua ya ahadi ya kununua nyumba – orodha ya wanaosubiri” waombaji wengine wa pili waliotimiza masharti ya kununua nyumba (20%)
 • Tangaza kufungwa kwa mchakato wa maombi ya mradi mahususi
 • Utumaji wa barua za kukataliwa kwa waombaji wengine wote wasiopangiwa nyumba
 • Marejesho ya fedha kwa waombaji waliopangiwa nyumba (na kukataliwa kuhawilishwa kwenye miradi mingine
 • Ukamilishaji wa malipo ya kiasi kilichobaki cha bei ya kununulia nyumba
 • Kubatilisha barua ya ahadi ya waombaji walioshindwa kukamilisha malipo yaliyobaki ya bei ya kununulia nyumba na kuwatumia barua ya ahadi ya kununua waombaji katika orodha ya wanaosubiri
 • Marejesho ya fedha kwa waombaji ambao barua zao za ahadi zimebatilishwa (na waliokataa kuhawilishwa kwenye miradi mingine)
 • Mchakato wa hati miliki ya nyumba
 • Kukabidhiwa nyumba.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015