Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Nifanyeje Kununua Nyumba
OFISI INAYOHUSIKA
Shirika la Nyumba la Taifa

THAMANISHA
Inafaa
()
Inafikika Kirahisi
()
 

Mtu anayekaa au kumiliki ardhi au eneo, majengo au nyumba iliyokodiwa kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa. Katika hali hiyo, mfumo wa kumchagua mpangaji ni seti ya vipengele ambavyo kila mmiliki ardhi mwenye busara ataviweka kutambua kukubalika kwa waombaji wanaotarajiwa.  Shrikika la Nyumba la Taifa limebuni mfumo mzuri utakaosaidia kuepuka kuchagua wapangaji kulingana na tukio na kutoa uamuzi utakaosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi na rushwa miongoni mwa wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa.  Kuwa na mfumo unaofaa wa kuchagua mpangaji  kutalisaidia Shirika la Nyumba la Taifa kuepuka wapangaji wenye matatizo na hivyo kuwa na uhakika wa kupata faida ya kutosha kutoka kwenye nyumba zilizopangishwa.

 Masharti:

 • Onyesha kipato chako cha sasa
 • Kodi iliyopendekezwa
 • Asilimia ya kodi kulingana na kipato
 • Kiwango cha kodi kilichoombwa
 • Uwezo wa kulipa kodi kabla
 • Uwezo wa kulipa dhamana ya kodi
 • Maoni ya wamilika wa ardhi waliopita
 • Fuatilia kumbukumbu ya historia ya mkopo
 • Sababu za kubadili makazi/ofisi
 • Ukubwa wa familia
 • Matarajio ya Ajira/matarajio ya biashara
 • Hali ya ndoa 

Taratibu:

 • Chukuwa ‘’Fomu ya Maombi ya Mpangaji’’ kutoka makao makuu ya Shirika la
  Nyumba la Taifa, ofisi yoyote ya mkoa au kupakua kutoka kwenye tovuti.
 • Jaza fomu ya maombi ya mpangaji kwa ukamilifu
 • Uwasilishaji wa fomu ya maombi ya mpangaji
 • Hakikisha kuwa taarifa yote muhimu/inayotakiwa imejazwa kwa usahihi
 • Lipa 5,000/= kama ada ya maombi.
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa: 19-11-2015